Skip to main content
best place to visit
Rudi kwenye Makala
4 dakika

Tanga kwa Macho ya Mwenyeji: Sehemu za Kutembelea

Tanga ina vivutio vingi; Mapango ya Amboni, Magofu ya Tongoni, pwani tulivu, na shamba la kilimo hai ambalo ni sehemu makini kwenye orodha ya lazima ya matembezi.

15 Machi 2026

Ukisikia neno "Tanga", wengi wanafikiria mji wa pwani tu — mahali pa kupita ukielekea Mombasa au Dar es Salaam. Lakini wakazi wa Tanga wanajua kitu ambacho wageni wengi hawajagundua: mji huu una kina cha raha zaidi ya inavyoonekana kutoka nje. Tanga Raha bwana! Asikwambiye mtu.

Bahari ya Hindi inakutana na nyanda za kijani milimani kaskazini mwa Tanzania. Hewa ni nyepesi, mji una historia ndefu ya Kiswahili na jamii za pwani, chakula cha baharini kinapatikana kila asubuhi. Lakini zaidi ya yote — Tanga ina utulivu! ambao unaonekana kupotea katika miji mingi ya pwani.

Makala hii imeandikwa kwa ajili ya mtu anayetaka kuitembelea Tanga kwa makini — si kwa haraka ya mtalii anayepiga picha juu juu na kuondoka. Hii ni orodha ya sehemu za matembezi au kujielimisha Tanga, zenye uzito, zinazostahili wakati wako.

Vidokezo vya safari: ziara za shamba Tanga · sehemu za kutembelea Tanga Tanzania · mambo ya kufanya Tanga · agritourism Tanzania

Tanga Banana Garden — Sehemu Inayobadilisha Jinsi Unavyoiona Tanga

Kuna sehemu moja Tanga ambayo si ya zamani, si maarufu sana, lakini inabadilisha jinsi utakavyohisi mji huu baada ya matembezi. Ni shambani, bustanini mwa Tanga Banana Garden. Utapata bidhaa fresh kama ndizi aina ya Cavendish, mkono wa tembo, kahawa, viungo na matunda mingine kama nanasi. — Hii ndio Tanga ya kijani kwa matembezi karibu na mjini.

Tanga Banana Garden ilizindua Kilimo cha kisasa kwa nia moja rahisi: kutoa nafasi kwa wapenzi wa mazingira kupumzika ndani ya mji, kupata maza fresh ya shamba yasiokuwa na kemikali, na kuelewa mazao ya shambani yanakotoka. Leo inakaribisha familia, vikundi vya wanafunzi, wapenzi wa mazingira asili , na wakazi wa kawaida wa Tanga wanaohitaji kupumulia hewa safi nje kidogo ya maisha ya mjini.

Tofauti na vivutio vingi ambavyo unaweza "kutembelea" kwa dakika thelathini, shamba hili linakualika uone furaha ya maisha na kilimo. Unatembea kwenye bustani ya migomba, utakatiza kwenye mikahawa, unaweza kuonja matunda yaliopandwa shambani

Harufu nzuri ya mimea, sauti, na mwendo wa polepole wa shamba — hizi ndizo zinazokufanya ukumbuke ziara yako Tanga.

•       Ziara za shamba zilizoongozwa kwenye — migomba, mikahawa na viungo

•       Kuonja kahawa ya Tanga iliyoandaliwa kiasili na wakulima.

•       Matembezi ya utamaduni yanayo kuunganisha na historia ya mkoa

•       Maeneo ya kupumzika yenye kivuli — bora kwa familia na picnic

Mapango ya Amboni — Siri Kubwa Zaidi ya Afrika Mashariki

Kilomita nane kaskazini ya mji wa Tanga, chini ya ardhi, kuna urithi wetu, ulimwengu mwingine. Mapango ya Amboni ni mfumo mkubwa zaidi wa mapango ya chokaa Afrika Mashariki — kilomita 234 za njia za chini ya ardhi, ingawa wageni hutembelea sehemu ndogo iliyoongozwa.

Mapango haya si ya kutazama tu — yana sauti yao, baridi yao, na nguvu yao ya kipekee.

Usisahau: Mapango ya Amboni yanafanya kazi vizuri sana kama ziara ya mchana baada ya matembezi asubuhi shambani. Unaweza kuanza Tanga Banana Garden saa mbili asubuhi, kisha ukazamia ndani ya Mapango ya Amboni mchana — safari kamili ya siku moja bila kwenda safari ya mbali.

Magofu ya Tongoni — Karne Saba za Ustadi wa Kiswahili

Upande wa kusini wa mji, karibu na pwani, kuna ukimya wa aina yake. Magofu ya Tongoni ni mabaki ya mji wa karne ya 14 — moja ya makaburi makubwa zaidi ya nguzo Afrika Mashariki. Nguzo hizi za marmar, zilizochongwa kwa ustadi wa ajabu, zimesimama kwa karne saba hadi leo.

Msikiti wa Ijumaa bado una kuta. Magao yake ya mawe yanasimulia hadithi ya biashara ya baharini, uislamu wa mapema pwani ya Afrika Mashariki, na ustaarabu ambao ulifika kilele chake Tanga kabla ya enzi ya ukoloni. Kwa watanzania wanaopenda historia ya nchi yao, Tongoni sio pakupakosa.

Jibu la swali la " Kwa nini nikazuru Magofu ya Tongoni? Unachohisi ukiwa pale — ukimya wa heshima, udongo wa historia, na uhalisi wa kwamba mji huu wa Tanga ulikuwa katika kitovu cha biashara ya pwani ya Afrika Mashariki.

Pwani ya Tanga — Amani Isiyo na Mithili

Pwani ya Tanga si ile ya kutathminiwa TripAdvisor wala ile ya vipeperushi vya safari. Tanga yetu hii 2026, haisumbui kwa msongano wa watu au magari. Mwendo ni wa aste aste. Maji ni shaba, wakati mwingine ya kijani kibichi, hii ni kwa sababu ya miamba ya matumbawe karibu — ni salama kwa kuogelea katika sehemu nyingi.

Watanzania wenyewe ndio wanaojua sehemu nzuri za kukaa pwani. Uliza mwenyeji wako wa hotelini au afisa usafiri — watakuelekeza mahali ambapo unaweza kupumzika bila kelele. Unaweza kwenda Tanga forodhani ukaunganisha na matunda fresh shambani Tanga Banana Garden.

Jinsi ya Kupanga Siku Nzima Tanga

Uzuri wa Tanga ni kwamba vivutio vyake vipo karibu. Unaweza kutembelea vitu vinne kwa siku moja bila haraka wala usumbufu wa masafa marefu.

Saa 2:00 asubuhi — Ziara ya shambani Tanga Banana Garden. Hewa safi na sauti ya ndege wa asubuhi shambani utaisikia. Tembelea bustani ya migomba ya ndizi na viungo kabla jua halijainuka juu. Halafu onja kahawa iliyoandaliwa na mkulima wa mtalaam.

Saa 5:00 asubuhi — Picnic bustanini au kuonja matunda fresh organic, ukipenda unaweza kuomba kuchukua nyumbani.

Saa 7:00 mchana — Endelea kusini hadi Magofu ya Tongoni kwa mwaka wa historia ya Kiswahili.

Saa 10:00 mchana — Mapango ya Amboni —Ziara ya mapango inachukua takriban saa moja na nusu.

Saa 12:00 jioni — Malizia pwani ya Tanga. Mwangaza wa jua la jioni linaonekana tofauti kabisa baada ya siku ya matembezi kama hii.

Uko Tayari Kutembelea?

Weka nafasi ya ziara ujionee mwenyewe

Tembea kwenye mashamba ya ndizi, onja kahawa safi ya Tanga, na ufurahie siku ya utulivu karibu na mji. Weka nafasi moja kwa moja au tupigie simu, nasi tutakusaidia kupanga ziara inayokufaa.

0702 666773
Tanga Banana Garden logo

Tanga Banana Garden ni shamba hai lililopo Tanga, Tanzania linalotoa ziara zinazoongozwa shambani, kahawa ya Tanga, matembezi ya utamaduni na ziara za kujifunza kwa familia, wasafiri na vikundi vya shule.

Chunguza

Nyumbani

Ziara

Kutuhusu

Makala

Wasiliana Nasi

  • Nyumbani

  • Ziara

  • Kutuhusu

  • Makala

  • Wasiliana Nasi

Mawasiliano

Tupate kwenye Google Maps

© 2026 Haki zote zimehifadhiwa.

Hakimiliki © 2026 Tanga Banana Garden. Haki zote zimehifadhiwa.